Serikali inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha silingi trilioni 32.4 katika bajeti ya mwaka 2018/19.

Hayo yamesemwa hii leo bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka 2018/19.

Amesema kuwa mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi trilioni 22 sawa na asilimia 68 ya mahitaji yote,

Aidha, Dkt. Mpango amesema kuwa shilingi trilioni 7.6 zitatumika kwaajili ya kulipa mishara ya watumishi wa serikali na taasisi za umma kwa mwaka huo hivyo kupunguza malimbikizo ya mishahara.

Akizumzia kuhusu deni la taifa, amesema kuwa limeongezeka mpaka kufikia dola 26,115,2 Juni mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 17 ikilinganishwa na dola 22,320.76 za Kmarekani mwaka uliopita.

 

Dkt. Kigwangalla aapa kuwashughulikia wala rushwa
Waliokosa mikopo watakiwa kukata rufaa