Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inafanya mapitio ya leseni zote za uchimbaji wa madini na zile ambazo zitabainika kuwa hazijafanya kazi kwa muda mrefu zitachukuliwa na kisha maeneo hayo hayo yatagawiwa kwa wachimbaji wadogo wadogo.
 
Amesema kuwa wizara ya madini imeimarishwa na sasa inatengeneza fursa kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu inayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Mji Mdogo wa Katoro.
 
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi katika Mji Mdogo wa Katoro uliopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Geita, akiwa kwenye siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
 
Aidha, amewaambia wananchi hao ambao wengi wao ni wachimbaji wadogo wadogo kuwa waendelee kuwa na imani na Serikali yao ambayo imedhamiria kuhakikisha wachimbaji hao wanafanya shughuli zao bila ya kubugudhiwa.
 
“Jipangeni kwa kufanya kazi, maeneo yapo na Serikali itawapa, nawashauri mjiunge katika vikundi vitakavyo sajiriwa na kutambulika kisheria ili muende kwenye mabenki mbalimbali na kukopa fedha za kununulia mitambo ya kisasa itakayo wawezesha kuchimba kwa kutumia teknolojia ya kisasa.”amesema Majaliwa
 
  • TCRA yataja wamiliki wa Wasafi TV, Kusaga hakutajwa
 
  • Video: Tumekusudia kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya Kilimo- Hasunga
  • Takukuru yamburuza mahakamani mtumishi wa DAWASA
Hata hivyo, Majaliwa ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Geita ihakikishe kila kijiji kinakuwa na kisima cha maji ili kuwapunguzia wananchi kutumia muda mwingi kwa kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji katika maeneo yasiyojulikana

Mbowe, Matiko wakwama tena, warudishwa rumande
Watumishi wawili wafukuzwa kazi TFDA kwa tuhuma za rushwa