Serikali imezindua mpango wa kuendeleza Viwanda vya mazao ya Kilimo utakaochochea Uchumi wa viwanda nchini na kuwanufaisha wakulima, mpango ambao umeandaliwa na Shirika la AGRA ili kusaidia kuinua sekta ya Kilimo. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na biashara, Profesa Riziki Shemdoe  amesema mpango huo ambao umelenga kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia Viwanda vya Kilimo ni muhimu kwa taifa hili hasa ukizingatia tupo katika uchumi wa kati na tunahitaji kufika mbali zaidi.

Aidha Profesa Shemdoe amesema kuwa andiko hilo litasimamiwa na mpango wa maendeleo ya Kilimo (ASDP11), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katibu Mkuu wa Kilimo kutoka wizara hiyo, Gerald  Kusaya amesema kuwa kupitia mpango huo Serikali inatarajia kufanya mapinduzi ya Viwanda yatakayoleta tija katika nchi

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Mifugo Profesa Elisante Ole Gabriel, amesema hivi sasa taifa linakwenda kutumia thamani ya bidhaa ambazo zinazalishwa nchini na kwamba mpango uliozinduliwa ni muhimu kwa taifa kwa kuwa lengo ni Tanzania kufika katika uchumi wa juu.

Tayari Wizara ya Kilimo imeshaanza kufufua Viwanda vya Kilimo ambavyo vilikuwa vikichakata Pamba, katika Mkoa wa Geita .

Serikali kuwainua wanawake wanaoishi vijijini
China, Urusi na Cuba washinda viti Baraza la Haki za Binadamu