Serikali ya jimbo la Lagos imetangaza mipango ya mazishi ya zaidi ya watu 100, waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga ukatili wa Polisi nchini Nigeria mwaka 2020 ikiwa ni mara ya kwanza kwa taarifa ya wizara ya afya kukiri kuwa serikali imekubali kuwa na idadi kubwa ya watu walifariki kufuatia ghasia hizo.

Vifo hivyo, vilitokea katika maandamano makubwa kuwahi kutokea ya #EndSARS yaliyoongozwa na vijana dhidi ya Serikali katika historia ya Nigeria, lakini yalimalizika kwa ukandamizwaji uliofanywa na vikosi vya usalama na mizozo mikali na kuzua maswali iwapo baadhi yao waliuawa kwa risasi na wanajeshi.

Ghasia wakati wa maadamanano huko Abuja, Oktoba 20 2020. Picha ya AFP.

Hata hivyo, Serikali ya jimbo la Lagos na vikosi vya jeshi vimekuwa vikikanusha kushiriki kuwafyatua risasi, kulenga eneo la Lekki lilipo lango la kulipia ushuru jijini Lagos, ambalo ndiyo kitovu cha maandamano hayo, huku jopo huru likisema waandamanaji hawakuwa na silaha.

Oktoba 20, 2020 kwenye lango la kulipia ushuru, na wengine waliuawa katika fujo na ghasia zilizozuka sehemu nyingine za jiji la jimbo hilo la Lagos huku Wizara ya Afya ya jimbo la Lagos ikisema waathirika 103 ambao miili yao imewekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa muda wa miaka mitatu bado haijadaiwa na familia, kwa hiyo itazikwa kwa pamoja hivi karibuni.

Robertinho: Nina kikosi imara sana
Moto wauwa 34 wakiwemo Wanajeshi 10