Serikali imesema inatarajia kukutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) kesho, ili kusikiliza malalamiko ya watumishi kuhusu nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 na kutoa ufafanuzi.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika kupitia ukurasa wa kijamii wa Twitter imesema kuwa serikali itakutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lengo likiwa ni kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara
“Ndugu wafanyakazi, Jumanne tarehe 26 Julai, 2022, serikali itakuwa na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi ili kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi kuhusu nyongeza ya mishahara katika mishahara ya Julai, 2022.”
Msemaji huyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kiwango cha fedha kilichoongezwa.
Moja kati ya mtumishi Mkoa wa Singida, Alfonce Daniel alisema ongezeko hilo limemshtua kwa sababu ni tofauti na alichokitarajia kutokana na kiwango cha mshahara wake.