Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatafakari namna yakufanya kazi na taasisi za dini bila kuwapa mzigo mkubwa wa tozo na kodi.
Rais Samia ametoa wito wa majadiliano baina ya Serikali na taasisi za kidini kuandaa mkutano kujadili namna bora ya kusaidia taasisi hizo kuendesha shughuli zake bila ya kulimbikiza madeni yatikanayo na tozo na riba.
Akizungumza na viongozi hao ikulu Jijini Dar es Salaam kuwa wazo lake ni kuwaandalia viongozi hao mkutano na Mamlaka ya mapato (TRA) kusudi wapate fursa yakuomba msamaha wa malimbikizo ya madeni yanayopelekea deni kushindikana kulipwa kutokana na riba na adhabu.
Aidha amesisitiza uadilifu pale misamaha hiyo itapotolewa na kukumbusha kuwa misamaha hiyo ilikuwepo toka awali ila ilisitishwa kutokana na kukosekana uadilifu na ubinafsi ukitajwa ni chanzo kimoja wapo.