Mgombea mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Samia Hassani amesema kuwa CCM itaendelea kuboresha huduma za afya kwenye maeneo yote nchini.kwa kujenga miondombinu ,vifaa tiba na kuongeza watumishi .
Akihutubia wananchi waliojitokeza kusikikiliza kampeni za chama hicho , Halmashari ya mji Nanyamba mkoani Mtwara , mama Samia amesema kuwa serikali itasisitiza matumizi ya bima ya afya ili kutoa huduma hiyo bila malipo ikiwa ni moja ya njia ya kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano .
“serikali itatongeza vituo vya kutolea huduma ya afya vingi kama inavyowezekana ,kama ilani yetu ilivyosema kujenga vituo vya afya kila katawahidi kwamba tutaendelea kujenga vituo vya afya katika kata zisizo navyo,” amesema Samia .
Aidha mama Samia amesema kuwa serikali inajipanga kujenga hospitali katika halmashauri 98 kwa yale maeneo ambayo hazijapa hospitali hizo .
Mgombea huyo wa CCM anaendelea na kampeni mkoani Mtwara ikiwa nikutafuta ushindi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.