Serikali ya Hispania itafanya kikao maalum cha baraza la mawaziri hii leo kutangaza hatua itakayochukua katika kuweka masharti dhidi ya jimbo la Catalonia.

Waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy amesisitiza kuwa serikali lazima iingilie kati kuhakikisha kunakuwa na utawala wa kisheria, wakati serikali ya Catalonia ilisema kuwa itatangaza kwa kauli moja uhuru wa jimbo hilo kutoka kwa Hispania.

Raia wa jimbo la Catalonia walijitokeza kupiga kura ya maoni ya kudai uhuru wa jimbo hilo lakini la serikali ya Hispania inasema kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika maandalizi ya kupiga kura ya maoni.

Kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont anasema amepewa mamlaka ya kutangaza uhuru wa Catalonia lakini sasa serikali kuu inakwenda kuchukua moja kwa moja nguvu na utawala wa jimbo hilo.

Kumekuwa na migogoro ya mara kwa mara tangu wacatalonia walipopiga kura ya kutaka kujitenga na Hispania na wiki chache zilizopita wahispania wanaopinga kujitenga kwa jimbo la Catalonia waliandamana mjini Madrid wakisema Hispania ni taifa moja na hawataki ligawanyike.

 

Serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Zitto Kabwe: Serikali ilikosea kujitangazia ushindi