Balozi wa Jamhuri ya Korea, Tae-ick Cho amesema kuwa Serikali ya Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takiwmu (NBS) kwa ajili ya kuimarisha miundombinu yake ikiwemo mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na kumalizia Ujenzi wa Ofisi za NBS katika Mikoa ya Dodoma na Kigoma.
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa leo Ijumaa (Julai 5, 2019) Jijini Dar es Salaam, Balozi Cho amesema Serikali yake ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika katika kuhakikisha kuwa NBS inatekeleza majukumu yake.
Balozi Cho amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Korea inatambua umuhimu wa takwimu katika shughuli za kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, hivyo itahakikisha kuwa mahitaji yote ya msingi kwa yanayohitajika na NBS ikiwemo uimarishaji wa miundmbinu ya TEHAMA inapewa kipaumbele.
Mwezi Juni mwaka 2018, tulianza mazungumzo ya ushirikiano na NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, hivyo utekelezaji wa masuala yote ya msingi katika mazungumzo hayo yapo katika hatua nzuri na nitawasiliana na Serikali yetu ili kuona jinsi ya kusukuma jambo hili kwa haraka zaidi,”amesema baloziĀ Tae-ick Cho
Aidha Balozi Cho ameongeza kuwa Serikali ya Korea itahakikisha kuwa makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa kwa haraka kwa kuwa inatambua ukubwa na umuhimu wa majukumu ya NBS katika uzalishaji na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya kuharakisha shughuli za Maendeleo ya wananchi.
-
Serikali ya Korea yaahidi kudumisha ushirikiano na Ofisi za NBS
- TTCL yaimarisha huduma zake, yavuna wateja lukuki
-
Dkt. Kolimba aviwezesha vikundi vya wanawake mkoani Njombe
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa NBS kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tayari ilianza hatua za awali za makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Korea na hivyo kupitia sheria ya misaada ambapo wameahidi kujenga na kuimarisha miundombinu ya Ofisi za NBS zilizopo katika Mikoa ya Kigoma na Dodoma.