Iwapo mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli atapata ridhaa ya watanzania ya kuunda serikali ya awamu ya tano, serilaki yake itanunua meli tano kubwa zitakazofanya kazi katika ukanda wa bahari ya Hindi.

Hayo yamesemwa na mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Bi. Samia Suhuhu alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mafia. Aliwahakikishia kuwa serikali ya CCM imejipanga kubadili maisha ya wakazi hao kiuchumi kwa kupitia sekta ya uvuvi.

Aliongeza kuwa ilani ya CCM imeainisha kuwa kila kijiji cha Mafia kitapata shilingi 1,000,000 ili kusaidia kuwainua wananchi hao kiuchumi, fedha hizo zitatumika katika kuwasaidia kununua vyombo vikubwa vya kufanyia shughuli za uvuvi.

Bi. Samia alisema mpango huo umelenga katika kuongeza ajira kwa wananchi wote hususan wakazi wa Mafia.

Kadhalika, alisema kuwa serikali ya CCM imepanga kununua meli nyingine 4 zitakazofanya kazi katika meneo ya Mtwara.

“Mafia mnastahili kuwezeshwa zaidi hasa baada ya kuonesha juhudi zenu kwa kujenga kiwanda cha samki lakini ilani yetu pia inasema tutanunua vyombo kwa ajili ya uvuvi ili kewnda katika ukanda wa kiuchumi wa bahari kuu na kuvua samaki wenye thamani kubwa.”

Ahadi Ya Lowassa Yafunika Kigamboni
Lowassa: Mungu Anipe Nini Miye…