Serikali ya Sudani na waasi wa kusini mwa nchi hiyo wamekuwa wakilaumiana kila mmoja kwa kukiuka makubaliano mapya ya amani ya nchi hiyo yaliyosainiwa wiki iliyopita.

Jeshi limekuwa likiwalaumu waasi kumuunga mkono Makamu wa Rais wa zamani, Riek Machar kwa kuanzisha mashambulizi katika jimbo la Upper Nile ambako raia 18 waliuawa.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, Lul Ruai Koang amesema kuwa waasi walishambulia mji wa Maban ulioko katika jimbo la Upper Nile karibu na mpaka wa Sudan, siku ya Jumapili.

Amesema kuwa majeshi yao yalijibu mashambulizi na katika mapigano hayo ambapo waasi waliwaua raia 18 na kuwajeruhi wengine 44. Miongoni mwa waliokufa ni raia watatu wa Ethiopia na wawili kutoka Sudan.

Hata hivyo, Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema kuwa hali bado ni ya wasiwasi katika eneo la tukio. huku watu bado wakihofia kurudi kwenye makaazi yao.

 

Mengi atoboa siri ya kutunga kitabu chake
Ubeligiji yafanya kweli