Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa naBalozi wa Ufaransa hapa Nchini Malika Berak, Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Aprili mwaka huu.

Berak amesema mkopo huo utaiwezesha na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na miradi ya umeme.

Kwa upande wake Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake hapa nchini kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya umaskini nchini.

Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande zote Mbili za Tanzania na Ufaransa.

 

Makamu wa Rais amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka kusaidia mchakato huo kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda nchini

Makalla atoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Jiji la Mbeya
Bil. 2,570.1 zalipia Madeni ya Ndani na Nje