Matumaini ya Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kushiriki fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ yamefufuka upya, baada ya Serikali ya nchi hiyo kuingilia kati.

Uganda ilikua kwenye hatihati ya kushiriki Fainali za ‘CHAN’ baada ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo ‘FUFA’ Moses Magogo Hassim kuthibitisha hali ya ukata.

Mapema leo Ijumaa (Desemba 16), Wizara ya Fedha nchini Uganda imetoa Shilingi bilioni 2 kati ya Shilingi bilioni 6 zinazohitajika kwa ajili ya Maandalizi ya Kikosi cha ‘The Cranes’ kitakachokwenda nchini Algeria kushiriki Fainali za ‘CHAN’ mapema mwaka 2023.

Wakati akitoa taarifa za Ukata Rais wa ‘FUFA’ alisema huenda kikosi chao kisishiriki Fainali za ‘CHAN’ kutokana na ukata wa fedha unaowakabili kwa sasa.

Taarifa nyingine zilieleza kuwa tayari Uganda ilikuwa imeshatuma Barua CAF ya kujiondoa kwenye Michuano hiyo, ambayo imepangwa kuanza kuunguruma Januari 13 hadi Februari 04 mwaka 2023.

Uganda imepangwa Kundi B lenye timu za DR Congo Ivory Coast na Senegal.

Kesi ya mauaji ya askari kusikilizwa machi 2023
Naibu Waziri Kigahe akabithi tuzo kwa wafanyabiashara