Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza azma ya Benki ya Biashara Tanzania (TCB) ya kuunga mkono juhudi za wajasiriamali wanawake hapa Zanzibar katika kukuza uchumi hasa uchumi wa Buluu.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Ikulu Jijini Zanzibar ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Beki hiyo Sabasaba Moshingi.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi amesema kwamba maono ya Serikali anayoiongoza ni kuubadilisha uchumi wa Zanzibar hivyo wadau kama Benki hiyo wanahitajika katika kufanya kazi pamoja na Serikali hasa katika kuwainua akina mama kiuchumi.

Amesema kuwa kusaidia akina mama ni jambo muhimu sana kwani hapa Zanzibar kuna kundi kubwa la wajasiriamali ambao wengi wao ni akina mama hivyo, kuna haja ya kuwaunga mkono hasa kwa wale wanaojishughulisha na ukulima wa mwani.

Ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kufanya kazi pamoja na benki hiyo kwani kumekuwa na mambo mawili ambayo yamekuwa yakiwakwaza wajasiriamali likiwemo dhamana pamoja na riba na ndio maana Serikali imeamua kwa makusudi kuingia makubaliano na benki ili iweze kuwasaidia.

Serikali, viongozi wa kidini kukutana
Afariki akifanya tendo la ndoa