Serikali ya Zimbabwe imeingilia kati sakata linalomkabili mke wa Rais wa nchi hiyo, Grace Mugabe, la kumshambulia mwanadada mmoja huko Afrika ya Kusini ikiomba mazungumzo ya Kidiplomasia yafanyike ili kumaliza kesi hiyo.
Grace Mugabe anayekabiliwa na kesi ya kumshambulia mwanadada mmoja mwanamitindo bado yuko nchini Afrika Kusini akikabiliwa na kesi ya kujibu, ingawa taarifa za awali zilisema kuwa alikuwa tayari karejea nchini Zimbabwe.
Aidha, mazungumzo bado yanaendelea kati ya mawakili wa mke wa Rais huyo wa Zimbabwe na ubalozi wa nchi hiyo nchini Afrika Kusini kuona namna ya kufanya mazungumzo ya Kidiplomasia ili kuweza kulimaliza tatizo hilo.
-
Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya azuiliwa Uwanja wa Ndege
-
Odinga kutinga mahakamani kupinga matokeo
Hata hivyo, Serikali ya Afrika Kusini itakabiliwa na shutuma kali endapo itamwachia huru mke wa Rais huyo, huku ikikumbukwa mwaka 2015 pia ilishindwa kumkamata nchini humo Rais wa Sudan, Omar el Bashir aliyekuwa anahitajiwa na mahakama ya ICC.