Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Serikali itawalinda wafanyabaishara wadogo wadogo maarufu kama machinga na kuhakikisha wanafanya biashara zao vizuri na kwa utaratibu mzuri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 5, 2021 Jijini Dodoma Msemaji Mkuu wa serikali Msigwa amesema kuwa serikali ipo kwa ajili ya kuhakikisha inaboresha mazingira ya kibiashara wafanyabiashara hao.

“Hakuna kwa namna yoyote serikali hii ya awamu ya sita inaweza kuwabagaza ama kutowajali wamamchinga,” amesema Msigwa.

“Muheshimiwa Rais ni Mama na kama ni mama angependa familia ziwe na amani usipowajali wafanyabiashara wadogo familia haziwezi kuwa na amani kwaivyo wafanyabiashara wadogo muw na amani,” ameongeza Msigwa.

Aidha Msemaji Mkuu wa Serikali Msigwa amewaasa wafanyabiashara hao kuendelea kufanya biashara kwa amani huku serikali ikiwa katika mchakato wa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara hao.

Waziri ummy aagiza wanaodai fidia kupisha Mto Ng’ombe waanze kulipwa
Serikali yatoa ufafanuzi mwanafunzi aliyejianika, "hakuchaguliwa, tunamtafuta"