Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua ili kukabiliana na upandaji wa bei za vyakula, hasa Mchele na Sukari.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wanaogiza vyakula nje ya nchi na watendaji wa Serikalini, wakati wa akifungua Tamasha la kwanza la Fahari ya Zanzibar na mwaka mmoja wa Taasisi ya Wakala wa Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi Zanzibar – ZEEA, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema, matarajio ya Serikali ni kurudisha bei za awali kwa bidhaa zilizopo madukani, pia ameagiza Serikali kutoa fedha zake za kigeni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara hususan waagizaji vyakula nje ya nchi, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana kuagiza bidhaa hizo kwa pamoja.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi pia amegusia suala la mizigo kushukia Bandari ya Mkoani akilenga kupunguza gharama za bidhaa Pemba, huku akitaka dola zitolewe kwa kuwapa kipaumbele Wafanyabiashara wa Bidha za Chakula, ili waweze kuagiza kwa wingi na apatiwe taarifa toka PBZ ni wangapi walioomba na wangapi waliopata.