Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.

Majaliwa amewataka watendaji wa halmashauri kuwa makini na matumizi ya fedha hizo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea zitamuunguza.

“Fedha hii tafadhali ni ya moto. Msicheze na hii ya halmashauri tunayoileta hapa halmashauri kwa ajili ya wananchi itawaunguza vidole. Tunaileta kwa madhumuni, tunataka wananchi wahudumiwe,“ – Majaliwa

Majaliwa ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 21, 2016) wakati akihutubia umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Azimio wilayani Mpanda.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri wahakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo yao kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

 

Audio: Lema amjimbu Waziri Nchemba kuhusu ‘kutotikisa kiberiti cha gesi’
Wassira aomba Serikali izungumze na Chadema yaishe, “Tatizo ni Lowassa”