Imeelezwa kuwa Ofisi ya Mkemia Mkuu Kanda ya Kati imepokea sampuli 36 zakupima vinasaba  vya kujua uhalali wa Baba wa watoto (DNA).

Hayo yamebainishwa leo mkoani Dodoma na Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati, Mussa Kuzumila wakati akitoa ripoti ya chunguzi zilizofanyika ndani ya miaka 2.

Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati, Mussa Kuzumila ameongeza kuwa, majibu yao husaidia kumaliza kesi mahakamani kwa wakati.

DNA ni vipimo ambavyo vinatoa ushahidi thabiti juu ya uzao wa mtoto, Baba anayedhaniwa kuwa baba mzazi anapimwa vipimo vya nasaba ili kuwa na uhakika kwamba yeye ndiye baba mzazi.

Nasaba hupatikana katika kiini cha seli hai na huwa na taarifa za urithi kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto, Taarifa za nasaba ndizo pekee zenye kutoa ukweli usiopingika kuhusu uzao wa mtoto.

Katika hatua nyingine Kuzulima amesema Kanda ya Kati wamepokea kwa wingi sampuli kutoka Jeshi la Polisi za Dawa za Kulevya hasa Bangi na Kokeini, kemikali.

Pilipili kutumika kufukuza Tembo kwenye makazi ya watu
Kocha Stars afungiwa CECAFA

Comments

comments