Serikali nchini imeondoa zuio la mabasi ya abiria kusafiri nyakati za usiku, huku Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi zikitakiwa kuweka utaratibu utakaofuatwa na wamiliki na madereva wa mabasi ya abiria wenye nia ya kusafiri nyakati za usiku.

Hayo yamebainishwa hii leo Juni 28, 2023 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Bungeni jijini Dodoma, na kuongeza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa zuio hilo lililowekwa miaka ya 1990 kufuatia matukio ya utekaji na udhalilishaji wa abiria.

Amesema, “itakumbukwa mwishoni mwa miaka ya 1990 serikali ilizuia mabasi ya abiria kusafiri usiku, zuio hilo lilisababishwa na matukio ya utekaji wa mabasi uliohusisha utekaji na udhalilishaji wa abiria, ajali mbaya za mabasi zilizogharimu maisha ya watu.”

Aidha, Majaliwa ameongeza kuwa changamoto za kiusalama na miundombinu zilizokuwepo kipindi hiko kwasasa zimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ambazo zitasaidia kufanikisha zoezi hilo kwa ufasaha.

Simba SC yafunguka Thank You ya Sawadogo
Ukubwa wa mafanikio ni kupambana - Dkt. Hezbon