Serikali nchini, imesema ucheleweshwaji wa fidia kwa wananchi unasababishwa na udanganyifu unaikuwepo kwenye maeneo husika huku luhga inayohusika kufanya udanganyifu ikiitwa ‘tegesha’ ambapo wakati wa tahmini unakuta mabadiliko kwenye eneo hilo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula leo April 24, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Ester Matiko aliyehoji ni lini Serikali itahakikisha inasimamia sheria za madini na Ardhi kuhakikisha kamba wananchi wanalipwa fidia yao stahiki ya kubomolewa nyumba na mazao.
Jamii, wakulima waingiwa hofu kasi ya gugu vamizi
Amesema “Serikali huwa inachukua picha za anga kabla ya kufanya zoezi na na inaangalia picha a nyuma kabla ya tahmini kuanza kulikuwa na nini na unapoanza tathimini unakuta kuna mali zingine zinaongezeka kama upandaji wa mazoao yanapandwa usiku na mchana”
Aidha Waziri Mbula amesema kuwa Serikali ina nia na dhamira njema hivyo kuwataka wananchi kuacha udanganyifu ambao unachelewesha haki za watanzania katika kulipwa fidia.