Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajani mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa oparesheni ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji.

“Sasa hivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapungua,”Amesema Ngonyani.

Aidha, amesema kuwa kutokana na wakulima hao wanaolima kando ya Mto kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi kunapelekea usalama wa maji hayo kupotea kwa watumiaji hivyo watu wafuate sheria ili kulinda maji ya Mto huo.

Serikali yalipa zaidi ya shil. bilioni 83 kwa wakulima wa Korosho
Video: Sumbawanga yashangaza Wasafi Festival

Comments

comments