Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amewaelekeza Viongozi wa Wilaya, Halmashari na wawakilishi wa wananchi kuimarishe ushirikiano baina yao na watumishi wengine, ili kuhakikisha azma ya Rais Dkt. Samia ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo inafikiwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa mkoa wa Songwe akiwa kwenye majumuisho ya ziara ya kikazi mkoani Songwe ya kukagua miradi ya maendeleo na mafanikio ambayo Serikali imeyapata, katika kipindi cha miaka miwili.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Waziri Kindamba (mwenye suti kulia)

Amesema, Viongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), pia wanatakiwa kuongeza wigo wa kufanya tafiti za maeneo ambayo maji yatapatikana sambamba na kuongeza ulinzi kwenye vyanzo vya maji ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa maji inatatuliwa.

Aidha, amewaagiza Wakaguzi wa Elimu nchini wapite kwenye shule zote wakakague vitabu vinavyotumika katika shule hizo kama vinaendana na maadili na tamaduni za Kitanzania na kusema, “Rais Dkt. Samia ameelekeza tusimamie maadili yetu, mila zetu, desturi zetu na utamaduni wetu wa Kitanzania.”

Wahamiaji 73 wahofiwa kufariki Pwani
Rais hatujali, hatuheshimu: Wanahabari