Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa mafanikio ya timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ ni matokeo ya uwekezaji kwenye mpira.

Timu ya Tanzanite kwasasa imeshawasili jijini Dar es salaam, baada ya kutoka kupeperusha Bendera ya Taifa nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya COSAFA na wamerejea na kombe hilo licha ya kualikwa.

“Wachezaji wetu wameonyesha namna uwekezaji unavyotoa matokeo chanya pamoja na kupeperusha Bendera kwa kujiamini ugenini ni jambo ambalo wanastahili pongezi,”amesema Shonza

Aidha, amesema kuwa kufanya kwao vizuri ni kitu cha kujivunia kwa Taifa kwani licha ya kualikwa wamerejea na kombe, lengo la Serikali ni kuhakikisha inafikia yale malengo ambayo imejiwekea, TFF pamoja na wadau.

“Kufanya kwao vizuri ni kitu cha kujivunia kwa Taifa kwani licha ya kualikwa wamerejea na kombe, lengo la Serikali ni kuona kila siku tunafikia yale malengo ambayo tunajiwekea, TFF pamoja na wadau ni muda wa kuwekeza kwa ajili ya baadaye,”amesema Shonza

 

Serena Williams aubwaga ubigwa kwa chipukizi wa Canada
RC-Moro azungumza baada ya majeruhi mwingine ajali ya lori kufariki dunia