Serikali imetoa imeisisitiza Klabu ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51% na mwekezaji anachukua 49%.
Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu hiyo na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.
“Kanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba 2017 ambapo ilioneka ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata muwekezaji basi mwekezaji achukue 49% na wanachama kutoka na mchango wao kwa mkubwa kwa klabu hiyo basi wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”amesema Dkt.Mwakyembe.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano haijaja kuua michezo bali lengo lake ni kuboresha michezo na kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hiyo.
-
Waziri Mwakyembe atembelea Serengeti Boys
-
Dkt. Mwakyembe awasihi Watanzania kumsaidia Wastara
-
Said Ndemla hang’oki Msimbazi
Naye Katibu wa Baraza la Michezo Taifa, Mohamed Kiganga amesema kuwa Ofisi yake ipo katika maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba ya kuwapa msisitizo wa Serikali katika kuzingatia sheria katika suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki ijayo.