Serikali nchini, inatarajia kutangaza ajira mpya 47,000 ikilenga kupunguza uhaba wa watumishi wa kada mbalimbali unaosababishwa na ujenzi wa miundombinu unaoendelea.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene hivi karibuni wakati akizungumuza na watumishi wa umma wilayani Chato, Geita.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.

Amesema, katika kuendelea kukabiliana na uhaba wa watumishi wa kada tofauti wa ofisi za umma, hadi mwezi Agosti 2023 Serikali imetoa ajira kwa watumishi 129,074.

“Serikali pia imepandisha vyeo watumishi 455,497 tangu ilipoingia madarakani mwezi Februari mwaka 2021 hadi Agosti 2023 na kufanya gharama za serikali kufikia Sh bilioni 84.3 kwa mwezi.” alisema.

DC Mtambule aongoza zoezi usafi wa Mazingira
Kamchape waingia kwenye 18 za Polisi Katavi