Ili kuongeza mazao mapya ya Utalii Nchini, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, inatarajia kukuza Utalii wa Fukwe, Mikutano na Utalii wa kuvinjari kwa Meli, kitu ambacho kitasaidia pia kuongeza idadi ya Watalii.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki katika hotuba aliyoitoa kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Saba ya Swahili International Tourism Expo – S!TE, 2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Ripoti ya Baraza la Utalii na Masuala ya Safari Duniani ya Mwezi Mei, 2022, imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 10 Bora Duniani kwa uhimilivu wa maeneo yake kupokea watalii Matunda ya hatua zinazochukuliwa na Serikali yanaonekana wazi.”

Aidha, Kairuki ameongeza kuwa mafanikio hayo yamepelekea, Sekta ya utalii kuchangia asilimia 25 ya fedha za kigeni, na asilimia 17.5 ya pato la taifa na kwamba sekta ya utalii imekuwa ikitoa ajira rasmi na zisizo rasmi kwa Wananchi.

Dereva wa Saibaba chanzo ajali iliyouwa saba Kilwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 7, 2023