Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde imekanusha juu ya zuio la mikutano na harakati za vyama vya siasa na kusema kuwa imeweka taratibu maalum kwa mujibu wa sheria kwa vyama vya siasa kufanya shuguli zake.
”Si kweli kwamba Serikali imezuia harakati za kisiasa, serikali haijakataza vyama kufanya harakati za kisissa lakini imeruhusu vyama kufanya kwa mujibu wa sheria na taratibu ambazo zimewekwa katika nchi yetu” amesema Mavunde
Ameongezea kuwa Msajili wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria amepewa mamlaka ya kuwa mlezi wa vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa matatizo yakitokea katika vyama anakuwa mstari wa mbele na sehemu ya kutatua matatizo hayo ili kuleta amani katika vyama vya siasa.
-
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 7, 2018
-
Mbowe awazungumzia madiwani 46 waliohama Chadema
Hayo yamezungumziwa bungeni pindi alipoulizwa juu ya kwa nini serikali imezuia harakati na mikutano ya kisiasa ili vyama visifanye kazi yake na kuhoji ni sheria ipi ambayo msajili inampa mamlaka ya kutengua vikao halali vya chama ambavyo vimefanywa kwa mujibu wa kanuni na katiba ya sheria ya nchi.
Aidha Agosti, 2016 jeshi la polisi lilipiga marufuku mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kote nchini kwa madai ya kwamba mikutano hiyo inatumika kuchochea uvunjifu wa amani.
Hatua hiyo ni kufuatia vikao vya ndani vilivyokuwa vinafanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye maeneo mbalimbali nchini katika maandalizi ya opreseheni waliyoiita ya kupinga udikteta Tanzania (Ukuta).