Serikali imekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao na kuchapishwa kwenye gazeti la Kenya la ‘The Standard’ kuwa rais John Magufuli amewafukuza wageni wanaofanya biashara nchini na kwamba serikali yake haitaki wageni kufanya biashara nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli na kwamba serikali haijawafukuza na haina mpango wa kuwafukuza wageni wanaoishi nchini wakiwa na vibali vilivyotolewa kisheri ana Idara ya uhamiaji.

Kadhalika, Bi. Kawawa alieleza kuwa kuna uzushi mwingine unaonezwa ukieleza kuwa rais Magufuli amepiga marufu wanawake kuvaa nguo fupi kwa madai kuwa ametoa amri hiyo kama sehemu za jitihada za kupiga vita maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Alisema kuwa rais Magufuli hajawahi kutoa amri hiyo na kwamba habari hizo zimezushwa na kuwataka wananchi kutoziamini.

Serikali imesema kuwa inatumia balozi zake za Kenya na Afrika Kusini kufuatili ili kufahamu chanzo cha habari hizo za uzushi.

Simba Waendeleza Ushindi Ligi Kuu Tanzania Bara
Samatta Arejea Lubumbashi Kumalizia Kiporo Chake