Serikali imelipongeza shirika la utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuendelea kurusha matangazo mubashara katika ziara mbalimbali za viongozi hapa nchini ikiwemo ziara ya Rais wa Jamhuri Misri hapa nchini.
Pongezi hizo zimetolewa mapema hii leo jijini Dar es salaam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan muda mfupi mara baada ya kuagana na Rais wa Misri katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.
Amesema kuwa shirika hilo la utangazaji linafanya vizuri ambapo limekuwa likihakikisha kuwa kila tukio kubwa limekuwa likirushwa mubashara hivyo kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa wakati muafaka.
“Niwapongeze sana TBC, kwani tangu jana tumekuwa pamoja kwenye mapokezi mpaka leo hii tena wakati wa kumuaga, hivyo hongereni sana na nampongeza mkurugenzi wa TBC kwa kazi nzuri anayoifanya,”amesema Samia Suluhu.
- Video: RC Makonda atoa msaada wa miguu bandia
-
Makamba: Serikali haitaruhusu tena kuuza shehena ya viroba iliyobaki
-
Mpina kukabiliana na changamoto za muungano
Hata hivyo, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limekuwa likihakikisha linarusha matangazo mubashara ili kuweza kuifikia jamii moja kwa moja, hivyo kufikisha ujumbe kwa muda muafaka