Serikali ya Afrika Kusini imepanga kumburuza mahakamani aliyekuwa rais wa wa nchi hiyo, Jacob Zuma kwa makosa ya ufisadi.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Shaum Abrahams amesema kuwa watamfikisha Zuma mahakamani kwa makosa 16 ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi.
Mashtaka hayo yanahusisha pia kiasi cha rand bilioni 30 (30bn rand au $2.5 bn) alizojipatia kinyume cha sheria, kwa kutumia ofisi ya Serikali tangu miaka ya 1990 kabla hajawa rais wa nchi hiyo. Mashataka mengine hanahusisha utakatishaji fedha.
Aidha, imeelezwa kuwa Zuma alitumia nafasi yake ya urais kuiomba rushwa kampuni ya Ufaransa iliyowekeza nchini humo.
Zuma alijiuzulu baada ya kushinikizwa na chama chake cha ANC ambacho kilitishia kumng’oa kwa kura ya kutokuwa na imani naye.