Bodi ya Filamu nchini, imemfungia muigizaji maarufu wa filamu, Wema Sepetu kutojishughulisha na uigizaji kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake chafu zilizosambaa mtandaoni.
Akizungumza wakati wa kutoa uamuzi huo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Joyce Fissoo amesema kuwa Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni na amekuwa akionywa na vyombo husika lakini amekuwa akirudia.
“Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii, na kwakuwa amekwisha onywa mara kadhaa safari hii tumeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu,”amesema Fissoo
Aidha, ameongeza kuwa kitendo kilichofanywa na msanii huyo kimeridharirisha taifa, jinsia, mashabiki wa kazi zake, hivyo kwakuwa amekiri kwa maandishi, itabidi atumikie adhabu mpaka pale serikali itakapojiridhisha kuwa amebadirika.
-
Serikali yamtaka Wema ajieleze
-
Wema: Nimefunga jalada la utoto, nimefunga jalada la ujinga, nimekuwa mpya
-
Makonda amvutia kasi Amber Rutty, amtaka ajisalimishe polisi
Hata hivyo, mapema jana Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambapo ilimuonyesha akiwa faragha na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa