Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imemtaka mkandarasi anayejenga Ofisi hizo Mjini Dodoma kukamilisha kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alipotembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi za Takwimu Mjini Dodoma, amesema kuwa kwa sasa NBS inatakiwa kuwa na Ofisi yenye hadhi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha shughuli za mbalimbali za takwimu nchini.
Amesema kuwa NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe hapa nchini ambayo imekuwa ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo linalopaswa kutimia haraka.

“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa,”amesema Dkt. Chuwa.

Aidha, Dkt. Chuwa amesema kuwa jengo hilo litakuwa ni la ghorofa tano na kwamba kwa kuwa wanazo Ofisi katika kila mkoa nchini, makao makuu hayo yatatumika kwaajili ya kuratibu uendeshaji wa shughuli za takwimu na mambo mengine ya maendeleo yanayohusiana na NBS.

Vilevile, Dkt. Chuwa amesema kuwa jengo hilo litagharimu sh. bilioni 11.6 hadi kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Hata hivyo,  Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Mtumwa Shomvi kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited, amesema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kusimamia mradi huo.

Didier Drogba Anunua Hisa Za Phoenix Rising FC
Jurgen Klopp Abadili Gia Hewani, Ataka Nafasi Za Ulaya