Serikali imebaini wizi wa umeme unaozalishwa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) uliofanywa na makampuni ya uwekezaji wa madini aina ya Tanzanite katika eneo la Mererani.

Mwenyekiti wa Kamati maalum ya Wizara ya Nishati na Madini inayopitia na kuhakiki mali zote za Tanesco, Mhandisi John Manyama alibainisha kuwa kamati yake imebaini wizi wa umeme wenye thamani ya shilingi milioni 157.6 katika eneo hilo.

Alisema kuwa uhakiki huo ulioanza Januari 4 mwaka huu ulibaini kuwa yapo makampuni 24 ya wawekezaji wa wazawa ambayo yamekuwa yakifanya wizi huo kwa kuchezea luku zao kwa njia tofauti tofauti.

“Shirika limeendelea kukosa mapato kwa ajili ya kuendesha shughuli zake za maendeleo kwa taifa kutokana na watu wenye nia ovu kama hawa wawekezaji. Kwa hapa mererani tumefanikiwa kufanya ukaguzi wa mita 163 na kati ya hizo tumekuta mita 24 zimechezewa kwa kiwango cha juu,” alisema Mhandisi Manyama.

Mhandisi Manyama alisema kuwa wamezichukua mita zote 24 za wawekezaji hao na watatakiwa kulipia faini tangu siku waliyofungiwa umeme.

Wananchi wauziana shamba la Sumaye, Sumaye mwenyewe azungumza
TV 6, REdio 21 zikiwemo za CCM, Diallo na Lowassa zafungiwa