Katika kuboresha huduma za afya, serikali imenunua mashine mpya za CT-Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.7, mashine hiyo inaelezwa kuwa na uwezo wa mkubwa wa kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.

Hayo yalibainika baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamisi Kigwangala kuitembelea hospitali hiyo jana na kudhuru idara ya magonjwa ya dharura, idara ya mionzi, na sehemu ya wagonjwa iliyo chini ya uangalizi maalum (ICU).

Mkuu wa idara ya Mionzi wa Hospitali hiyo, Dkt. Flora Lwakatare alisema kuwa mashine hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Siemens ilifungwa siku mbili zilizopita na tayari imetumika kutoa huduma kwa wagonjwa 26.

“Mashine hii inatoa huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo, tumbo, kifua na inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” ¬†alisema Dkt. Flora.

Naye Dkt. Kigwangala alieleza kuwa mashine hiyo imenunuliwa kwa fedha za umma na sio mkopo.

 

Polisi Wamkamata Kijana aliyejichora michoro ya ajabu na jina la Yesu
Simba Ashindwa Kuunguruma Kisiwani Unguja