Serikali nchini, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi tayari imetenga Shilingi Bilioni 4.4 katika programu ya vituo atamizi kwenye vituo vinane (8) kote nchini kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifyugo Tanzania (TALIRI).
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde, wakati wa ziara ya kutembelea vituo atamizi vya Wizara hiyo Mkoani Tanga vinavyotekelezwa kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI).
Amesema, hadi Mwezi Machi mwaka huu ng’ombe 865 kati ya 900 wamenunuliwa kwa ajili ya programu hiyo ambayo mpango wa mafunzo ni mwaka mmoja na kila kijana atapata fursa ya kunenepesha mifugo hasa ng’ombe.
Aidha, Silinde ameongeza fursa hizo pia ni kuwa katika mizunguko minne ya ng’ombe kumi (10) kwa kila mzunguko na faida itakayopatikana baada ya kuuza ng’ombe hao itatumika kama mtaji kwa ajili ya kijana mnufaika kwenda kuanzisha miradi kama hiyo.