Ikiwa leo ni  siku ya wajane Duniani kituo cha msaada wa  sheria kwa Wanawake na watoto (WLAC) imeitaka Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ya mirathi ya Kimila kwani ni kandamizi na inawanyima haki wanawake na wasichana.

Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC Theodosia Muhulo amesema kuwa Serikali inatakiwa kuharakisha Mchakato wa Katiba mpya ili kuhakikisha kwamba haki zilizoanishwa kwenye Mkataba wa CEDAW zinapewa kipaumbele dhidi ya vifungu visivyowiana vya sheria ya Mirathi ya Kimila ambayo ni ya kibaguzi.

Mnamo 2013 Kituo cha Msaada wa Sheria WLAC kushirikiana na wadau wengine hususani Kliniki ya Kimataifa ya Haki za wanawake ya Kituo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Georgetown iliwasilisha taarifa kwa kamati ya Mkataba wa Kimataifa kwa kamati ya kuondoa aina zote za Ukatili dhidi ya wanawake (CEDAW) kuhusiana na kesi na namna ambavyo wajane wamekiukiwa haki kisheria.

Bi. Muhulo ameongeza kuwa pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanywa na WLAC na wadau watetezi wa haki za wanawake, bado serikali haijaonesha jitihada za maksudi kutekeleza maamuzi ya kamati ya Mkataba wa CEDAW kuhusu sheria ya Mirathi ya Kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba wanapatiwa haki zao stahiki.

Magufuli Asitisha Ajira Kupisha Zoezi la Uhakiki wa Watumishi Hewa
Mtoto wa Michael Jackson afunguka baada ya picha ‘chafu za watoto’ kukutwa chumbani kwa Michael