Serikali imewaonya watu wanaojihusisha na kusambaza maudhui mitandaoni ikiwemo video fupi zinazohimiza uhusiano wa jinsia moja kitu ambacho ni kinyume cha tamaduni, mila na desturi.

Onyo hilo, limetolewana Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jijini Dar es Salaam na kusema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imebaini uwepo wa baadhi ya watazamaji wa maudhui hayo ya kulipia mtandaoni.

Amesema, ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kusambaza maudhui hayo hata kama yanalenga kuelimisha, badala yake wanapotumiwa video hizo wanatakiwa kuzifuta na si kuzisambaza.

Rangi zinazotajwa kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja.

Naper ameongeza kuwa, Serikali imepanga kuwachukua hatua kali kwa wanaoongoza makundi ya mitandao ya kijamii ambao wanachama wao wamekuwa wakishawishi kitendo hicho kwa kusambaza maudhui hayo.

“Kiujumla anga letu la mtandao liko salama kwani TCRA wapo kazini kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa salama na hata inapotokea kuna maudhui hasi na yanayokiuka sheria, inachukua hatua stahiki kwa wanaohusika kwa kushirikiana na vyombo vya dola hasa jeshi la polisi,” amesema Waziri huyo.

Hata hivyo, amewasihi Wazazi, Walimu na Walezi kuwa na wajibu wa kuwalinda watoto wao kutokana na maudhui yasiyofaa hasa yanayorushwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo huchangia upotofu.

Kocha Mtibwa Sugar aitisha Young Africans
Parimatch na fursa ya 'namba zina hela cheza Bingo'