Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya maji kwa kutekeleza miradi mikubwa katika sekta hiyo, kama ilivyopangwa na kuelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo akifungua Kongamano la Maji Zanzibar linalofanyika Mkoa wa Mjini Magharibi na kuongeza kuwa dira hiyo pia ni ile ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, ahadi alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa na Jumuiya za kikanda na Kimataifa.

Amesema, “Serikai itaendelea kuimarisha sekta ya maj kwa kutekeleza miradi mikubwa kama livyopangwa na kuelekezwa kwenye llani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, kufuatia ahadi dizoziloa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.”

Aidha,, Rais Dkt. Mwinyi pia ametoa wito wa kuvisimamia vyanzo vya maji na kuhakikisha vinalindwa ili kuepusha uvamizi pamoja na kuandaa utaratibu wa utambuzi wa maeneo na kuyapatia hatimiliki kwa uendelevu wa vyanzo hivyo huku akiwataka wasimamizi wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na watafiti.

TSB kuimarisha masoko ya ndani uzalishaji zao la Mkonge
Hawajui wanachotakiwa kukifanya - Rais Samia