Serikali imepanga kuzalisha mitamba zaidi ya milioni 1 kwa mwaka ili kukuza sekta ya mifugo hapa nchini na  kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ambapo amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa uchumi na ustawi wa wananchi.

“Vituo vya uzalishaji vilivyopo Arusha na Sao Hill Iringa vimeboreshwa ili viweze kutoa mbegu bora za kutosha kwa kufanya maboresho makubwa katika vituo vya kanda vya uzalishaji mbegu za mifugo,” amesema Mpina

Amesema kuwa kuelekea uchumi wa viwanda, Serikali imejipanga kuzalisha mifugo mingi ya kutosha ili kupata bidhaa bora zitokanazo na mifugo.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali imevunja mikataba na wawekezaji wengi ambao hawakuweza kutimiza malengo ya uwekezaji katika sekta ya mifugo.

Hata hivyo, katika kuboresha sekta ya uvuvi Waziri Mpina amesema wafanyabiashara watumie fursa ya kuzalisha nyavu halali ili kuchochea ukuaji wa sekta ya uvuvi kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya bidhaa za uvuvi.

Jeshi la Marekani lakamata silaha Ghuba ya Aden
Video: Tazama matamasha ya ajabu yanayofanywa na wazungu