Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amepiga marufuku uhamisho holela wa watumishi pasipo kuzingatia maslahi ya uhamisho, kwani utaratibu huo unavunja moyo utendaji wa watumishi wa umma.
Shigella amesema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, kwa mkoa wa Geita, na kuelekeza kuwa taratibu za uhamisho lazima zifuatwe.
Amesema, “marufuku kumhamisha mfanyakazi kama bado bajeti ya uhamisho haipo, hayo ni amelekezo ya Rais, mkijua mnahamisha wafanyakazi kadhaa wekeni kwenye bajeti zenu, labda kama ameomba mwenyewe.”
Aidha, Shigella pia ameagiza taasisi za umma na binafsi kuhakikisha wanazingatia stahiki za wafanyakazi wanapokuwa kazini kwa muda wa ziada, kwani ni matakwa ya kisheria na ni haki kwa mtumishi na kukemea tabia ya wafanyakazi kutolipwa malimbikizo yao.
Chanzo: Habari leo.