Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jami, jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu kwa niaba ya Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye jumla ya shilingi bilioni 3.2 kutoka kwa wadau mbalimbali, makampuni binafsi, na wadau wa maendeleo katika kuunga mkono jitohada za Serikali kupambana na Corona hapa nchini.
Ambapo Waziri Ummy amepokea fedha zilizowasilishwa kwa mfano ya hundi zenye thamani ya shilingi 3,185,500,000 na vifaa kinga na tiba vilivyotolewa na Taasisi ya Lotary Club ya Bahari Beach jijini Dar es salaam vyenye thamani ya shilingi 15,000,000.
Akipokea misaada hiyo Waziri Ummy amesema misaada hiyo itaelekezwa zaidi na Serikali katika kuongeza kununua zaidi vifaa kinga kwa ajili ya wataalamu wa afya ambao wako mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja nakuwezesha utoaji wa mafunzo zaidi kwa wataalamu wetu ambao wanapambana usiku na mchana ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wahusika na wagonjwa wa corona.
Ametaja kampuni zilizohusika katika kutoa msaada huo wa mabilioni ya fedha ikiwa ni pamoja na Kampuni ya SAN & LAM iliyotoa shilingi 172,500,000, FAIDA -Letshego BANK Shilingi 33,000,000, Financial Sector Depending Trust 225,00,000, VODACOM Shilingi 2,300,000,000, TUICO TAIFA, 10,000,000, Kampuni ya SONGAS 100,000,000 na Shirika la Reli la Tanzania 65,000,000 na Benki ya NBC.