Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa madawati 300 toka Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kutatua tatizo la uhaba wa madawati katika shule za msingi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri wa Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Maiga kwa niaba ya serikali alisema kuwa amesema kuwa kupokea madawati hayo ni sehemu ya kutekeleza wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

“Waziri Mkuu alitutaka sisi katika nafasi zetu tuwashirikishe wadau mbalimbali ili kuweza kutekeleza adhma ya serikali ya kutatua tatizo la wanafunzi kukaa chini ili waweze kupata mazingira bora ya kupata elimu, alisema Balozi Maige.

Balozi Maigaaliongeza kuwa Kuwait iko tayari kuisaidia nchi ya Tanzania kwa kuwajengea uwezo wataalam toka Tanzania kwa kuwapa elimu ya mafuta na gesi kwani Kuwait ina uzoefu mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi.

Naye Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jaseem Al Najem alisema kuwa Serikali ya Kuwait itaendelea kutoa misaada kwa serikali ya Tanzania kadri itakavyowezekana pindi pale itakapohitajika.

Aidha Balozi Maiga alitumia muda huo kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  ujio wa Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini siku ya Julai Mosi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya  kikazi.

“Rais wa Rwanda atawasili hapa nchini Julai Mosi na ataweka saini makubaliano mbalimbali waliyofikia kati ya Tanzania na Rwanda baada ya hapo Rais Kagame ataambatana na mwenyeji wake Rais Magufuli mpaka katika viwanja vya maonesho vya Sabasaba ambapo Rais Kagame atayazindua rasmi maonesho hayo ya arobaini”, alisema Balozi Maiga.

Aidha Balozi Maiga aliongeza kuwa Rais Kagame jioni atakaribishwa Ikulu na mwenyeji wake Rais Magufuli kwa ajili ya dhifa ya kitaifa

NEMC Yaboresha Mchakato Tathmini Ya Mazingira Nchini
Zaidi ya Watu 30 Wauawa Libya