Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba wa kuanzisha Kituo cha Huduma za Binadamu na Operesheni za Dharura cha Kanda ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo hii leo Aprili 5, 2023, wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Amesema, “katika kuendeleza uhusiano na nchi nyingine, nchi yetu imeungana na mataifa mengine kutoa misaada ya kibinadamu kwa nchi zilizopatwa na maafa yaliyosababisha vifo na majeruhi, uharibifu wa mali na mazingira. Nchi hizo ni Malawi iliyokumbwa na kimbunga Freddy Machi 13, 2023 na Uturuki iliyokumbwa na tetemeko la ardhi Februari, mwaka huu.”

Ameitaja misaada iliyotolewa kuwa ni Malawi kuwa ni tani 1,000 za mahindi, mablanketi 6,000, mahema 50, fedha taslimu sh. milioni 705, dawa za binadamu na helikopta mbili kwa ajili ya kusaidia uokoaji. Vilevile, Uturuki ilipewa dola za Marekani milioni moja.

Serikali yaunda Madawati 1,393 ulinzi, usalama wa Mtoto
Mbadala wa Onyango asakwa Simba SC