Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali itahakikisha haki inapatikana kwa wananchi wote bila kujali hadhi ya mtu, uchumi wala kabila na itaendelea kufanya maboresho ya kiutendaji na ujenzi wa miundombinu, ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Mahakama na kuimarisha mifumo ya utoaji haki.
Majaliwa ameyasema hayo mapema wiki na kuongeza kuwa katika mwaka 2022/2023, Serikali imekamilisha miradi ya ujenzi wa Mahakama tatu za hakimu mkazi katika Mikoa ya Lindi, Songwe na Katavi.
Amesema, “aidha, ujenzi wa Mahakama za Wilaya 28 katika Wilaya za Same, Mwanga, Tandahimba, Nanyumbu, Namtumbo, Mvomero, Gairo, Ngara, Kilombero, Mkinga, Kakonko, Buhigwe, Uvinza, Butiama, Rorya, Itilima, Busega, Mbogwe, Nyang’hwale, Kyerwa, Misenyi, Tanganyika, Kaliua, Manyoni, Bunda, Kilindi, Rungwe na Sikonge umekamilika.
Waziri Mkuu amebainisha kuwa, pia ujenzi wa Mahakama ya mwanzo katika Wilaya ya Kilindi eneo la
Kimbe na ukarabati wa Mahakama Kuu ya Tabora pamoja na Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi umekamilika.