Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka wahitimu wa Chuo cha Afya K’S kilichopo Jiji la Mbeya, kwenda kuitumikia Jamii kwa uzalendo na Upendo kwani Serikali imewekeza kwenye Huduma bora za Afya Nchini.
Akizungumza kwenye Mahafali ya nane ya Chuo hicho, Malisa amewakumbusha wajibu wao kama Wataalam wa Afya kuwa, jamii inawahitaji hivyo ni vyema kutumia lugha za upendo katika kuwahudumia wagonjwa.
Kwa Upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Norbert Sizari ameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ushirikiano wa na kuwapatia Wanafunzi fursa ya mafunzo kwa Vitendo.
Mapema wiki hii, Serikali pia iliwataka Wauguzi wa kada ya Utabibu, Wakunga na Wauguzi nchini, kutumia mitandao ya kijamii vizuri bila kwenda kinyume na maadili ya fani yao, na kuacha kutumia lugha chafu na kejeli kwa wagonjwa ili kuheshimisha kada hiyo.