Wizara ya Madini imesema kuwa imesitisha mnada wa madini aina ya Tanzanite uliokuwa umetangazwa kufanyika katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani Manyara tarehe 12 hadi 15 Oktoba 2017.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa umma imesema kuwa kuahirishwa kwa mnada huo kunatokana na kuridhia kwa maombi ya wadau wa mnada ambao waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki kwa wingi.

Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa  uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa Mererani.

Hata hivyo, Wizara ya Madini imewaomba radhi wadau wote wa Sekta hiyo ndogo ya madini ya vito hususani Tanzanite ambao wameathirika kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huo..

Video: Chris Brown aachia ngoma mpya yenye masharti kuitazama
Sheikh Ponda atii amri ya RPC Mambosasa