Serikali imetaifisha madini ya Almasi yenye thamani ya shilingi Bilioni 61.97 yaliyokuwa yanatoroshwa na waliokuwa watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwenda Nchini Ubelgiji kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Waliotorosha madini hayo yenye uzito wa kilogramu 14.33 ni aliyekuwa Mkurugenzi wa uthaminishaji madini na vito (TANSORT), Archard Kalugendo na aliyekuwa mtathimini wa madini ya almasi wa Serikali Edward Rweyemamu.

Aidha madini hayo yametaifishwa baada ya mahakama ya Kisutu kutoa hukumu dhidi ya washtakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kuisababishia serikali hasara ya dola 29,509,821.84.

Sambamba na kutaifisha madini hayo, mahakama pia imewapiga faini ya shilingi milioni 1 kila mmoja na kama watashindwa kulipa faini watatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.

Yemen yaomba msaada wa kuwatenganisha mapacha walioungana
Majaliwa aipa TPA wiki 2 Bandari ya Kagunga itoe huduma