Kufuatia zoezi linaloendelea la oparesheni kamata mifugo linaloongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Luhaga Mpina, serikali kwa mara nyingine imetaifisha kundi la ng’ombe 171 waliokamatwa katika kijiji cha Kakere wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Mpina amesema kuwa Wilaya zilizopo mipakani mwa nchi jirani ziko katika tishio kubwa la kuvamiwa na mifugo, hivyo amemuelekeza mwanasheria wa Wilaya ya Kasulu kuanza kuandaa utaratibu wa mahakama kuzipiga mnada ng’ombe hizo.

“Hatua ya kwanza sisi kama Serikali tunataifisha ng’ombe hawa na kufanya utaratibu wa kuzipiga mnada na mwanasheria wetu wa Serikali aanze taratibu ambapo ng’ombe hao tutawapiga mnada kwa mujibu wa sheria ya magonjwa ya wanyama No. 17 ya mwaka 2003.” amesema Mpina.

Aidha, amesema kuwa ng’ombe hao kwa sasa wataendelea kuwa chini ya Serikali mpaka taratibu zitakapo kamilika na kuitaka  kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kasulu  kuelendelea kwa kasi kubwa kukamata mifugo katika mapori na kuhakikisha mifugo yote inapatikana.

Hata hivyo, kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanahawa Mrindoko amesema kuwa ng’ombe hao waliokamatwa ni mali ya raia wa Rwanda, ambapo amesema kuwa sheria itachukua mkondo wake.

 

Video: Chadema yazidi kumong'onyoka, Hatima ya hekalu la Mch. Rwakatare leo
Hamilton anyakua taji la nne la Formula 1