Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza kukamilisha taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa Serikali wa wilaya ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji, ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe 6648 walioingia nchini kinyemela toka nchi jirani ya Uganda.

Mpina amesema kuwa uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la ng’ombe linaweza kusababisha madhara makubwa katika mazingira kama vile mmomonyoko wa ardhi, uharibifu wa vyanzo vya maji.

“Sisi kama Serikali hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee na mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina jukumu la kuhakikisha tunalinda rasilimali hii ya malisho,” amesema Mpina.

Aidha, Mpina ameongeza kuwa suala hili haliingiliani na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwani Ushirika huo upo kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo kinyemela nchini toka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine.

Kwa upande wa upande wake mkuu wa wilaya ya Misenyi, Kanali Denis Mwila amesema kuwa zoezi la kutathmini ng’ombe katika wilaya yake bado linaendelea na taratibu za kisheria zinafuatwa.

Hata hivyo, akiwa Mkoani Kagera, Mpina ametembelea mabwawa ya mradi wa samaki yaliyopo Wilayani Muleba katika kijiji cha Luhanga na kusema Serikali ina nia ya kukomesha kabisa uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wavuvi haramu kule waliko.

Zitto awapigia magoti Watanzania
Usimamizi wa rasilimali wazidi kumpaisha JPM